Germain, Muuzaji wa magari kule Yaounde, Cameroon
Germain ni muuzaji wa magari ambaye anafanyia kampuni iitwayo SOCADA katika viunga vya mji wa Yaounde. Nilikuwa na tashwishi nilipokuwa nikipiga picha hii, Germain alipokuwa anajibu simu yake ambayo hulia mara kwa mara, kuwahudumia wateja wake mara hiyo hiyo na kuwapa maelezo wafanyikazi wenzake. Alifaulu kupata namna ya kupiga picha karibu na Peugeot 407.